Arsenal, Manchester United yaungana na Spurs kuwania saini ya nyota wa Ivory Coast

C0DgWluXEAEq1eL

Tottenham Hotspur ndiyo klabu ya kwanza kutoka nchini Uingereza kutuma ofa rasmi ya kuitaka saini ya kiungo wa Atalanta inayoshiriki Ligi Kuu nchini Italia, Serie A Franck Kessie.

Spurs imeweka mezani £19m lakini inatajwa kwamba United, Arsenal na Chelsea wameingia vitani kuiwania saini ya nyota huyo kutoka nchini Ivory Coast kwa dau la €23m.

Taarifa kutoka mtandao wa ESPN zinaeleza kwamba United ipo katika nafasi nzuri ya kuinasa saini ya Kessie kwa kuwa mwenyewe angependa kujiunga na timu hiyo.

Kiungo huyo amekuwa na msimu mzuri baada ya kufunga mabao sita na kutoa pasi mbili za mabao kwenye michezo 16 msimu huu.

Kessie alijiunga na Stella Club ya nchini humo mnamo Mwaka 2015 kabla ya kutolewa kwa mkopo na msimu huu kuibukia Atalanta anapoendelea kufanya vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *