Alliance yavutwa shati nyumbani, Singida yazidi kujisafishia njia Ligi Kuu

Alliance_v_Mgambo


Alliance Academy ya Mwanza imeendelea kupotea njia katika mbio za kusaka tiketi ya kupanda Ligi Kuu baada ya kulazimishwa sare nyingine ya mabao 1-1 na Panone uliochezwa leo katika uwanja wa nyumbani wa Alliance.

Alliance ilitangulia kupata bao kupitia kwa Judy Philemon dakika ya saba ya mchezo huo  lakini walishindwa kulilinda na kujikuta Panone wakisawazisha bao hilo katika dakika ya ishirini kupitia kwa John George.

Kwa matokeo hayo, Alliance inayofundishwa na Kocha John Tegete imetimiza pointi 22 na kujikuta imezidiwa pointi 3 na vinara Singida United waliofanikiwa kuifunga Mvuvumwa bao 1-0.

Wiki iliyopita Alliance ililazimishwa sare na vibonde Mgambo na sasa baada ya sare ya leo imebakiza mechi moja tu ya nyumbani dhidi ya Rhino Rangers.

Matokeo mengine katika ligi Daraja la kwanza yameshuhudia Kiluvya United ikiibamiza African Sports 4-1 huku Polisi Moro ikiitambia JKT Mlale kwa kuitandika mabao 2-0

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *