Alexis Sanchez athibitisha kufanya maamuzi magumu

Alexis Sanchez

Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez amesema ameshafikia uamuzi wa mustakabali wake msimu ujao.

Pamoja na kufanya maamuzi ya klabu atakayoichezea msimu ujao, mshambuliaji wa Chile hakuwa tayari kuweka wazi kama atabaki Arsenal au kujiunga na timu mojawapo zinazomhitaji ikiwemo Manchester City.

Sanchez, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao yupo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Chile kilichotinga Fainali ya Kombe la Shirikisho. Katika mahojiano na kituo cha Sky Sports News HQ, Sanchez amesema kwa sasa akili yake iko katika Kombe la Shirikisho.

” Swali zuri. Kwa sasa nafikiria zaidi Kombe la Shirikisho, nitaangalia kama nitabaki au kuondoka baada ya kumalizika kwa mashindano haya.”

Alipoulizwa kama ameshafikia uamuzi wa atakaoenda msimu ujao, alijibu kwa kucheka, ” Naam, hilo liko bayana lakini siwezi kukuambia. ”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *