Al Ahly waushukuru ubalozi kwa kukamilisha upelelezi wa Yanga

Niyonzima_Alhly

Mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya soka ya Al Ahly ya Misri Syed Abdul Hafiz amemshukuru balozi wa Misri nchini Tanzania mheshimiwa Yasser Shawwaf kwa jitihada kubwa zinazofanywa na Ubalozi wake uliopo hapa nchini kwa kile kinachosemekana ni kazi ya kipepelezi.

Ubalozi wa Misri nchini Tanzania umesema utahakikisha unawatumia Al Ahly mikanda ya video zote za michezo ya Yanga kadiri watakavyoipata ili kuwasaidia Al Ahly kuweza kuzisoma mbinu za Yanga.

“Dhumuni kuu la Kuwatumia mikanda hiyo ni kuwasaidia benchi la ufundi kujua udhaifu na Uimara wa Yanga” alisema balozi huyo ambaye anafanya mawasiliano na makampuni ya Ndege kwa ajili ya kuzifikisha video hizo mapema na haraka iwezekanavyo.

Al Ahly kwa sasa wanaangalia jinsi gani watapata unafuu wa usafiri hapa nchini Tanzania vile vile hoteli nzuri watakayofikia pamoja na uwanja wa kufanyia mazoezi.

Al ahly wanatarajia kuumana na ya Yanga tarehe 9 mwezi Aprili mwaka huu katika hatua ya 16 bora ya Ligi Ya Mabingwa barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *