Bayern munich kuwakabili Mainz leo

Mabingwa mara tatu mfululizo wa ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga, Bayern Munich wanajitupa uwanjani leo kumenyana na klabu ya Mainz katika Dimba lao la nyumbani la Allianz Arena.

Wachezaji wa Bayern wakishangilia

Wachezaji wa Bayern wakishangilia

Siku chache zilizopita Bayern Waliichapa Wolfsburg mabao 2-0. Mchezo wa kasi na wakuvutia ndio umekuwa silaha ya bayern msimu huu.

Ushindi huo dhidi ya Wolfsburg ulikuwa ni wa tatu mfululizo na umewapa pointi nane zaidi ya Borussia Dortmund wanaoshika nafasi ya pili.

Kwa upande wa Mainz wao waliibuka na Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao Bayer leverkusen katika uwanja wa Cocafe Arena.

Ushindi huo umewasogeza Mainz mpaka nafasi ya tano, pointi moja juu ya Leverkusen katika msimamo wa ligi ya Bundesliga.

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza leo
Bayern Munich (mfumo 4-1-4-1): Neuer; Lahm, Kimmich, Alaba, Bernat; Alonso; Robben, Müller, Costa, Coman; Lewandowski.

Mainz (mfumo 4-2-3-1): Karius; Donati, Balogun, Bungert, Bussmann; Baumgartlinger, Frei; De Blasis, Malli, Jairo; Cordoba .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *