Yanga v Mwadui: Tegete, Nizar uso kwa uso na mabosi wa zamani

Licha ya mvuto wa asili wa mechi za watani wa jadi zinapokutana toka enzi na enzi lakini mvuto unaongezeka zaidi pale inapotokea mchezaji aliyewahi kuwika upande mmoja anapohamia upande wa pili na timu hizo kukutana.

Mechi iliyopita , Hamisi Kiiza aliyetakata vilivyo na Yanga msimu huu akiwa Simba SC alitazamiwa kuleta upinzani mkali na wakali hao wa Jangwani lakini safu ya ulinzi ya Yanga SC ilisimama imara kuhakikisha mwajiriwa wao wa zamani haleti madhara langoni mwao.

Jumatano hii Yanga inarudi tena kibaruani kwenye Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara huku ikikabiliwa na mtihani wa kuwazuia wachezaji wake wa zamani kuizamisha meli ya timu hiyo ambayo kwa sasa inakata mawimbi kwa kasi kubwa.IMG_8974

Mashabiki wa soka nchini wanakumbuka Akida Makunda baada ya kuwahama Simba SC na kutua Jangwani aligeuka mwiba mkali sana kwa wekundu hao.

Anakumbukwa sana kwa krosi zake zenye macho hususani mechi ya 1996 pale Kirumba ambapo Simba walilala kwa mabao 3-1. Hapa utaona ni jinsi gani wachezaji makini wanapohamia upande wa pili hugeuka mwiba.

Nizar Khalfan al maarufu kama kiungo mstaarabu aliachwa msimu huu na wana Jangwani hao baada ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi hicho na hii ilitokana na kuporomoka kwa kiwango chake .

Lakini kwa sasa Nizar ni nguzo imara ya Julio pale Mwadui. Yanga wanahitaji kucheza kwa tahadhari na mchezaji huyu ambaye anajiamini, uzoefu na uwezo mzuri kusimama kiungo cha juu au kucheza kama kiungo wa pembeni.

Bila shaka wengi watakuwa wakimtafakari Jerry Tegete na kasi aliyonayo kwa sasa. Pia watakuwa wanalikumbuka baoalilofunga Miraji Athumani Jumatano iliyopita dhidi ya Yanga. Kifupi Jerry ni mshambuliaji kiasilia.

Anapokuwa kwenye kiwango cha juu na akachezeshwa vizuri basi ana nidhamu zote za mshambuliaji kutumia nafasi za wazi na hata kutengeneza .

Kama Ally Mustapha ‘Barthez’ na safu yake ya ulinzi itarudia makosa yale kwa Tegete kuna uwezekano shujaa huyo wa Taifa Stars enzi hizo akairarua timu ya mabosi wake wa zamani.

Yanga SC wategemee upinzani mkali sana kwa Mwadui inayoundwa na wazoefu na damu changa ukizingatia ipo chini ya kocha Julio ambaye bado ana hasira na Yanga SC waliompiga mabao 8-0 msimu uliopita akiwa na Coastal Union.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *