Ukaribu wangu na wachezaji umetupa kombe la Ligi Kuu – Conte

Kocha mkuu wa mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza msimu huu , Antonio Conte ametanabaisha ukaribu wake na wachezaji wake ndio umewafanya jana kutawazwa kama mabingwa wa ligi kuu nchini England.

Alikuwa ni Batshuay kunako dakika ya 82 alipoifungia Chelsea goli la ushindi akitokea benchi goli ambalo lilidumu mpaka kipenga cha mwisho .

Akihojiwa na waandishi wa habari baada ya mchezo huo Conte raia toka nchini Italia , alisema ukaribu wake na wachezaji wa timu hiyo toka awasili klabuni hapo ndio umempa ushindi usiku wa jana .

” “Every game I feel like I have played with my players. I show my passion and my will, my desire to stay with my players in every moment of the game. This is me,” Conte said.

“In the present, in the past, I stay with my players in positive and negative situations. We won this title together.”

Alitanabaisha kuwa karibu na wachezaji katika kila mchezo na kuna wakati alijiona ni kama alikuwa akicheza nao uwanjani mbali ya kusimama kama mwalimu mazoezi na kiongozi katika benchi la ufundi.

Conte anakuwa kocha wa nne wa kitaliano kuipa ubingwa wa timu ya ligi kuu nchini England akitanguliwa na wenzake Ancelotti, Roberto Mancin na Claudio Ranieri aliyefanya hivyo msimu uliopita dhidi ya Leicester City.

Heshima kubwa aliyojijengea Conte kwa wachezaji ndio siri ya mafanikio yake na hilo lilionekana jana baada ya mchezo kwa wachezaji wote kumkumbatia na kuimba naye nyimbo za furaha kusheherekea ushindi huo.

Conte amejiunga msimu huu wa ligi kuu akipokea kijiti toka kwa mholanzi Guus Hiddink na umekuwa msimu wake wa kwanza wa mafanikio kwa kuwapa kikombe matajiri hao wa London.

Na Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *