Tathimini mchezo wa leo kati ya Simba v Stand United

Ilikuwa tarehe 2 Novemba mwaka jana kabla ya kumalizika Kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu pale Shiza Kichuya katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga alipowainua wana msimbazi kwa goli la jioni la penati na matokeo kutamatika kwa 1-0.

Leo atarudia ? au Stand kulipa kisasi?

Baada ya dibaji hiyo fupi tuanze tathimini yetu kwa kuziangalia timu zote mbili katika nyanja mbalimbali na mchezo husika kwa ujumla.

KISAIKOLOJIA
Tukianza na Simba SC ; wanaingia katika mchezo huu wakiwa vyema kisaikolojia dhidi ya Stendi United. Walishinda mchezo wa awali dhidi yao kule Shinyanga pia wameshinda michezo 19 katika ligi tofauti na Stendi walioshinda mechi 8 tu kati ya 28 walizocheza .Hili pekee linawafanya Simba SC waingie uwanjani wakiwa na uhakika wa kusaka ushindi .

Mchezo uliopita dhidi ya African Lyon Simba walicheza vizuri na kuibuka na ushindi wa goli 2-1 hivyo watahitaji kuendeleza wimbi la ushindi ili kujiweka vyema katika mbio za ubingwa ambazo mpaka sasa zipo rehani kwa timu zote mbili yaani Simba SC na Yanga SC.

Simba wanatambua kupoteza mchezo wa leo ni kuwafungulia njia wapinzani wao wakubwa Yanga SC kuibuka mabingwa wa ligi kuu kwa kuhitaji mechi moja tu kati ya mbili walizonazo. Hili litawafanya kuingia uwanjani wakiwa watulivu kisaikolojia ili wasipoteze mchezo huo na kugeuka mbeleko ya ubingwa kwa wanajangwani.

Tukija kwa upande wa wageni wa jiji Stendi United ni kama wanakuja kukamilisha ratiba . Licha ya kujinadi kushinda mchezo wa leo kulipiza kisasi kwa mechi ya awali wakiilalamikia sana penati ya Kichuya lakini siwaoni katika hali ya ushindani zaidi kama walivyo Simba SC .

Wapo nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu tayari wakiwa na alama 35 ambazo zinawapa uhakika wa kubaki ligi baada ya zaidi ya timu 8 chini yake zinapambama kuwafikia ili wasiungane na JKT Ruvu kushuka daraja.

Kinachowapa dira ya mapambano ni kulipa kisasi au kutafuta alama moja kujihakikishia zaidi kubaki ligi kuu hivyo watacheza kwa kujilinda zaidi kuliko kufunguka dhidi ya Simba.

KIUFUNDI NA KIMBINU

Simba SC wana faida kubwa katika hili . Ni moja ya timu ambayo ipo vyema kimfumo ndani ya ligi kuu kutokana na mafundisho ya mwalimu Omog na msaidizi wake Jackson Mayanja.

Wamekuwa wakifanya vyema na mfumo wa 4-4-2 au 4-3-3 dhidi ya wapinzani wao. Matumizi ya walinzi wanne nyuma , viungo wanne na washambuliaji wawili wamekuwa moto wa kuotea mbali hususani safu ya kiungo na wings zao.

Kulia Besala Bukungu amekuwa msaada mkubwa katika marking na kuanzisha mashambulizi ya kasi . Ni mchezaji ambaye anapigiwa upatu zawadi ya mchezaji bora wa kigeni . Tazama alipoumia Simba ilikuwa haiko sawa bawa la kulia na hakika Kichuya aliikosa back up yake licha ya Hamadi Juma kujaribu kuvivaa viatu vyake.

Zimbwe jr kushoto ana consistency nzuri akiwa Ni mchezaji wa Simba SC alicheza takribani mechi zote . Kifupi Simba wapo vyema eneo la ulinzi hata wakati huu wanapomkosa mlinzi wao wa kati Methodi Mwanjali bado kiungo mkabaji James Kotei anatengeneza kombinesheni nzuri na Lufunga .

Stendi watatakiwa kuwa makini eneo la kati la Simba SC ambalo ndio husimama kama roho ya timu kushambulia na kujilinda . Jonasi Mkude na Mzamiru Yassini wameanza kuelewana vyema na kuifanya timu kuwa na utulivy mzuri pia matumizi ya viungo wakabaji kama walinzi wa kati inaongeza idadi ya viungo kwenye timu na kuwapa nguvu nzuri kwenye kumiliki mpira na kukaba. Viungo wa Stendi Ngalema , Selembe , Jackob Masawe , Mayanga na Adamu Kingwande itawahitaji kuwa makini.

Goli la Ibrahimu Ajibu mechi iliyopita dhidi ya African Lyon linakuonesha uwezo binafsi wa mchezaji husika katika kuipatia timu matokeo. Walinzi wa kati wa Stendi wana kazi ya ziada kuizuia kasi ya Simba SC kwenye safu ya ushambuliaji ambayo kimsingi inapewa nguvu kuanzia kati na kwenye wings.

Ajibu au MO Ibrahimu na stereo type. Ni wachezaji ambao wana uwezo mkubwa katika kumiliki mpira , kukokota na kufunga au kuwafanyia wenzao screening kama play makers na kufunga hivyo Stendi wana kazi ya ziada kuukata mfumo huu wa uchezaji wa Simba SC aidha kwa kuziba njia kuanzia eneo la kati na kuwakabia juu mawinga wa timu hiyo pia walinzi wao katika kuanzisha mashambulizi.

Shiza Kichuya ana goli 11 katia msimamo wa ligi na wamebakiwa na mechi mbili tu hivyo atafanya kila awezalo kutafuta njia ya kufunga ili ajiweke vyema katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu . Saimoni Msuva yupo kileleni akiwa na goli 13 tofauti ya goli 2 tu. Mahitaji binafsi ndani ya timu wakati mwingine huongeza ari na kiu ya kutafuta ushindi .

Tukimalizia na Stendi United kimbinu; ni dhahiri watatumia mfumo wao wa siku zote wanapokutana na timu zilizo juu kiuwezo dhidi yao . Walipocheza na Yanga kule Kambarage walitumia 4-2-3-1 wakaibuka na ushindi wa 1-0 goli likifungwa na Pastory Athanasi ambaye sasa yupo Simba SC .

4-2-3-1 ni sawa na 4-5-1 au 4-1-4-1 . Ni mfumo ambao unatoa uwiano mzuri katika kushambulia na kujilinda pia . Stendi watahitaji zaidi ya viungo wakabaji wawili pale kati kupambana na viungo wa Simba SC . Muunganiko wa Mkude , Mdhamiru na Ajibu inakupasa uwe na watu wa kazi kuwakataa sivyo timu yako itapwaya .

JUMLA

Kwa ujumla wake mchezo utakuwa wa ushindani dakika 15 za mwanzo na baada ya hapo tutajua nani atajipanga kumzuia mwenzake na nani atakuwa mshambuliaji.

Hali ya hewa leo jijini Dar inaruhusu mchezo kucheza katika hali nzuri tofauti na mechi zilizopita ambazo zilichezwa kwenye mvua .

Pressure ya upinzani wa Mbao FC ambao Simba wanakutana nao kwenye fainali ya kombe la ASFC mei 28 , itawafanya leo kutulia sana kuibuka na ushindi ili kujiweka kwenye hesabu za ubingwa vizuri kotekote

 

By Samuel Samuel

10 Comments

 1. baby gate plastic

  June 4, 2017 at 9:50 am

  Would things have been easier with one?

 2. Syreeta

  August 19, 2017 at 7:10 pm

  It is a rare opportunity to see the 2000 years old Swayambunath which
  a Buddhist Chaitya. Goa is among the most desired holiday destinations as it spells uninhibited fun.
  In my student days, airlines exacted baggage fees by charging by the pound for “overweight” luggage.

 3. Inbox Blueprint

  August 27, 2017 at 12:53 am

  And that is the rationale, Anik Singal is again with an even bigger and higher Inbox
  Blueprint 2.0 course that will help you make it massive with
  Email Marketing.

 4. https://bloodynightgown.tumblr.com

  November 1, 2017 at 10:07 am

  Regardless of what the temperature is outside, inside the hive it
  must remain a constant 95 deg. The Honey Pot Strategy is regarding the
  placement of items with good traffic generating products.

  Manuka honey Elixirs may also be an all natural soothing formulation for dry throats.

 5. White matte Lipstick

  February 4, 2018 at 5:26 pm

  Hello, this weekend is good in support of me, as
  this occasion i am reading this impressive informative article here at my house.

 6. Matilda

  February 12, 2018 at 10:01 pm

  I’ve never pondered %BT% in this manner. Thanks author, it was
  very worthwhile to read! I really wanted to have such wonderful penning abilities but I
  am terrible at it. This might be a heavy trouble but there are can be found
  special critique online resources, such as
  the one you can visit by clicking on this link Matilda, where qualified writers and reviewers review different writing services to help those who are hunting for educational writing support.

 7. Buddy

  March 3, 2018 at 3:16 pm

  Hello to every body, it’s my first pay a quick visit of
  this webpage; this blog includes remarkable and
  genuinely fine stuff designed for readers.

 8. Define işaretleri hakkında herşey

  June 2, 2018 at 11:37 pm

  I’m impressed, I have to admit. Rarely do I come
  across a blog that’s equally educative and entertaining,
  and let me tell you, you’ve hit the nail on the head. The issue
  is something that too few men and women are speaking intelligently about.

  I am very happy I came across this in my search for something concerning this.

 9. new mobile Casinos 2016 Uk

  July 24, 2018 at 12:17 pm

  This exciting Las Vegas casino has you covered.

 10. Nichol

  August 1, 2018 at 2:45 pm

  Icch muss bei Ihnen dafür bedanken diese fantastischen lesen !!
  Ich auff jeden Falll absolu liebte bisschen es.
  I habwn Buch-Kennzeichnung Sie bitte zuersst neue Sachen, die Sie veröffentlichen …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *