Shtuka Kavumbagu, mshike bega na Oscar Joshua

Ni kweli wanasema mafahali wawili hawakai zizi moja. Ni msemo wa kiswahili ukitanabaisha ukinzani wa nguvu kwa miamba miwili na mwisho wa yote lazima utengano utokee.

Lakini pia wahenga walikuna tena vichwa na kuibuka na msemo “kila mfalme na zama zake”.

Soka ni taaluma endelevu inayohitaji utayari kinadharia na vitendo muda wote kwa ngazi zote . Mfano, ni lazima mchezaji apate elimu kuhusu maisha yake ya soka muda wote na elimu hiyo inakaa vyema kichwani mwake endapo anapata muda wa kutosha kuifanyia kazi hususani kucheza mara kwa mara.

Tukisimamia hilo basi wadau wa soka ni lazima wapate tafsiri mbadala ama mtambuka na misemo ya wahenga hususani usajili unapofanyika ndani ya timu. Ni dhahiri shahiri tunafanya usajili kutokana na mahitaji kimfumo, kimbinu na masuala yote ya kiufundi.kavumbagu1

Pia kwa soka la kisasa hata hitaji la kiuchumi hutupelekea kufanya usajili ili kutokana nahadhi ya mchezaji husika ili kunufaika kibiashara hususani mauzo ya jezi na mambo mengine kama kuvutia mashabiki uwanjani.

Falsafa hii ya uhitaji kwa baadhi ya wachezaji imegeuka anguko kuu katika soka lao na vipaji kwa ujumla. Mfano mwalimu anapofanya usajili wa kiungo namba 6 baada ya kumuona aliyepo hatoshelezi au yupo peke yake, shida inakuja pindi yule anaekuja kupewa kipaumbele kwa karibu michezo yote na kumtelekeza kabisa huyu aliyemkuta ni sawa?

Kimbinu na Kisaikolojia mchezaji makini kukosa mechi 10 mfululizo ni maumivu makali sana. Ni athari Kisaikolojia na kuua ukuaji wa kipaji chake. Sasa kuna wengine wanakaa benchi nusu msimu au kuishia kucheza msimu mzima mechi tatu tu.

Mantiki ni nini? tujifunze kuwaachia kama hatuna mahitaji nao ingawa kwa wachezaji wasiojitambua yupo radhi kukaa tu kwa sababu yupo timu kubwa.

Lakini kwa upande mwingine ukilitazama kiufundi suala hili unaweza pata jibu kwa namna moja. Waalimu wengi kwa sasa si wazuri kukuza vipaji vya wachezaji . Wanajuakufanya kazi na wachezaji wenye vipaji binafsi vilivyo komaa. Lakini uwezo wachezaji unapopungua hawana uwezo wa kumrudisha mchezaji katika ubora wake kama sio juhudi zake binafsi.

Haiwezekani mchezaji akawa bora msimu uliopita halafu msimu huu akaonekana galasa kabisa. Nenda kamuulize Tambwe falsafa kama hajakupiga ngumi na ambacho Simba walitaka kumjengea kichwani.

Hapo ndipo kwa sauti kubwa nasema “Shtuka Kavumbagu, mshike bega na Oscar Joshua”

Lakini pia waalimu tufahamu jambo moja , kuna baadhi ya mbinu na mifumo tunatumia ambayo ina kinzana na aina ya wachezaji tulio nao . Vijana wengi sikuhizi wanajifunza soka sio vipaji asilia kuweza kunyumbuka na mbinu zozote zile.

Tusiue ndoto zao kwa mbinu zetu wenyewe. Mwisho ni utayari wa mchezaji husiku kujibidiisha muda wote ili kulinda ustawi wa soka lako. Nidhamu binafsi na nidhamu ya mpira wa kisasa.

One Comment

  1. Tori

    May 20, 2017 at 11:04 am

    Ceci dit, honneur au journaliste d’investigation Günter Wallraff ! L&iniuo;isvestqgatron, c’est précisément ce qui manque trop souvent en France, à part quelques rarissimes exceptions à C+. C’est là où on voit l’abaissement où est rendu le journalisme dans notre pays.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *