Mkude kukosa penati Simba inahusika vipi?

Nguvu tunazotumia kuzigawa timu za taifa kwa Usimba , Uyanga na dhana mpya ya Uazam ni sumu ya maendeleo kwa soka la nchi hii.

Sumu hiyo inaua saikolojia za wachezaji wetu ndani ya timu hizo nakuwafanya muda wote wanakuwa kwenye msongo wa mawazo. Mkude kukosa penati Simba inahusika vipi?

Mkude_01

Timu ya Taifa, Taifa Stars ilipotolewa na Algeria kuna baadhi ya watu walipeleka lawama kwa Yanga na Azam kwa wingi wa wachezaji toka timu hizo. Tutafika lini ?

Katika mapambano yoyote yale unapovurugwa Kisaikolojia ni rahisi kushindwa kwa kukosa utulivu licha ya maandalizi.

Sumu hii imetutafuna kwa miaka mingi na inazidi kuota mizizi. Hatujui tatizo letu la msingi. Tunataka kukimbia wakati kutembea hatujui.

Tuliomba makocha wazawa lakini nao tunawananga kila uchao.

Mkwasa_kibadeni

Kibadeni licha ya kukipanga kikosi vizuri jana na timu kuonekana ipo vyema lakini baada ya kutolewa kwa matuta naye yamemkuta ya Mkwasa. ” kajaza simba watupu ”

Tutafute maziwa tuitapike hii sumu kisha tujue tatizo la msingi ili japo tusonge mbele. Soka lina misingi yake ambayo kiuhalisia kwa miongo kadhaa tumeivuruga kwa makusudi.

Hebu fungua macho ya kisoka na ujionee kuanzia ngazi ya vilabu na kitaifa kwa ujumla tunajiandaa kwa soka baadae?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *