Hatumuoni Donald Ngoma?

Dakika 29 baada ya mechi ya Yanga SC na Azam FC ikiiendelea, nilikuwa ndani ya uwanja wa taifa nikishuhudia mechi hiyo na jopo kubwa la wadau wa soka nchini.
“Hivi Samuel huyu Donald Ngoma baadhi ya washambuliaji wetu walioko timu ya taifa na vilabu vyetu wanajifunza lolote lile toka kwake?”

Ilikuwa ni sauti ya mwenyekiti wa Yanga Facebook Family na katibu mkuu wa Taifa Stars Supporters ndugu Josephat Sinzobwakila.

Nilitabasamu kisha nikamwambia , “Mkuu nchi hii ina mambo mengi mazuri sana tatizo ni jinsi ya sisi wazawa kujua thamani ya kuyatumia kwa maendeleo yetu ya sasa na kesho”.
IMG_3823
Tunahitaji kina Ngoma zaidi ya 20 nchini. Mchezaji mwenye nidhamu kubwa ya soka uwanjani , uwezo wa kutumia nafasi adimu kufunga, uwezo wa kuubadilisha mchezo , uwezo wa kuilazimisha safu ya ulinzi ya wapinzani kumtizama yeye tu na kuwaruhusu wengine kuwa na mwanya wa kuwa huru kufanya watakalo (keep them busy).

Nikimtazama Donald Ngoma nakikumbuka kizazi cha dhahabu cha akina Nteze John, Mmachinga, Golota , Mwamba Kizota na wengineo ambao walijua vyema matumizi ya nguvu zao na akili kuipa timu ushindi.

Hatuna muda wa kuwaangalia kina Diego Costa, Rooney na wakali wengine majuu lakini huyu yupo hapa tunapigana nae vikumbo vipi hakuna la kuchukua toka kwake?

Nafahamu tumejaa unazi na dhambi ya kuamini anachofanya yule unayemhusudu ndio bora maana kuiga mema kwa adui kwetu ni msamiati.

Haya yanamfanya kiungo wa Coastal Union kutopata hata wasaa kuzitazama vipande vya video za Ndemla au Juma Abdul kujiuliza kuna kitu naweza pata kwa Kwao?

Ukiangalia msimamo wa wafungaji wa mwaka jana utaona majina ya akina Kamuntu na Mandawa lakini msimu kasi imepungua . Ni kweli bado mapema lakini tabia ya kujifunza mbinu mbalimbali kwa watu mbalimbali inasaidia kukuza kipaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *