El Clasico: Nani kuibuka mbabe?

maxresdefault_26

Kila mmoja anaweza kuwa na mawazo yake tofauti maradufu juu ya El Clasico, winga wa zamani wa Real Madrid, Steve McManaman amesema kwama “El Clasico si mchezo kama ulivyo mchezo wa Everton dhidi ya Liverpool au Manchester United ambao unaonekana kuwa na wapinzani wengi”.

Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 70 ya mabao ya Barcelona kwenye La Liga yamefungwa na washambuliaji wake hii ikiwa ni asilimia kubwa kuliko timu zote za La Liga.

Real Madrid mabao yake mengi msimu huu yamefungwa na walinzi wa timu hiyo, inawezekana Zidane anaingia kuwakabili Barcelona bila presha yeyote msimu huu kwa kuwa hana cha kupoteza tofauti na Luis Enrique atakayekuwa na deni kubwa la kuwafurahisha mashabiki wake baada ya kufungwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa na kutupwa nje.

Hii ni mechi ambayo huvuta hisia za wapenzi wengi wa soka duniani huku sababu kubwa ikiwa ni katika mechi hii maarufu kama el clasico ndipo wachezaji wawili bora duniani Christiano Ronaldo na Lionel Messi wanapokutana.

El Clasico ni jina lililobeba uhalisia wa mchezo wenyewe, yaani mchezo bora. Unaweza kuita ‘Classic’ kama jina lenye maana sawa na hilo. Jina hili awali lilikuwa likihusisha michezo ya Barcelona na Real Madrid pale walipokutana kwenye La Liga pekee, yaani Ligi Kuu ya nchini Hispania. Baadae waliamua kuuita jina hilo kila timu hizo zilipokutana.

Uhasama wa Barcelona na Real Madrid unaanzia kwenye siasa, itakumbukwa tangu miaka ya1930 na 1936 ambapo Barca kama ndio walizaliwa upya waishi upya maisha mapya. Mpaka sasa Katalunya haina mapenzi makubwa ya dhati na Hispania. Hii ni sababu nyingine inayochochea ladha ya mchezo huu.

Nani kuibuka na ushindi leo?

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza.

Real Madrid: Keylor Navas, Dani Carvajal, Sergio Ramos, Nacho Fernandez, Marcelo, Toni Kroos, Luka Modric, Casemiro, Asensio, Cristiano Ronaldo, Karim Benzema.

Barcelona: Ter Stegen, Gerard Pique, Samuel Umtiti, Jordi Alba, Sergi Roberto, Sergio Busquets, Ivan Rakitic, Andres Iniesta, Lionel Messi, Paco Alcacer, Luis Suarez

One Comment

  1. Jessie

    May 20, 2017 at 5:47 am

    Will, thanks for your comments and pass on my best wishes to Elli. I look forward to seeing her myself hopefully very soon, well I can wish can’t I&s2830;?Raje#h ; )

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *