Antonio asaini mkataba mpya

Kiungo mshambuliaji wa West Ham United Michail Antonio amesaini kandarasi mpya ya miaka minne na klabu yake mpaka mwaka 2021.

Antonio mwenye umri wa miaka 27 aliondoka mwezi wa nne mwaka huu kwenye kikosi cha timu yake na kikosi cha timu ya taifa ya England baada ya kuumia vibaya mguu wake majeraha ambayo yamemuweka nje ya uwanja mpka mwisho wa msimu .

Kabla ya kuumia , Antonio alikuwa akiongoza kwa ufungaji katika klabu yake akiwa na magoli 9!. kitu ambacho kimeushawishi uongozi na benchi la ufundi la timu hiyo kuingia nae mkataba mwingine mpaka 2021.

Akizungumza na mtandao wa klabu hiyo baada ya kuingia kandarasi hiyo mpya , Antonio alisema haya ;

” nimekuwa nikifurahia maisha hapa . Nashukuru Mungu mambo yamekwenda vizuri na tumeingia mkataba mpya . Klabu hii imenipa fursa ya kuitwa kwa mara ya kwanza kuichezea timu yangu ya taifa jambo ambalo lilikuwa ni ndoto yangu toka nikiwa mtoto” alieleza kiungo huyo ambaye anaendelea kuuguza majeraha yake.

Antonio amekipiga na kikosi cha Slaven Billic kocha mkuu wa West Ham United kwa mechi 69 toka ajiunge na kikosi hicho msimu wa 2015-16 akitokea Nottingham Forest .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *