Yanga itafakari kuondoka Kwa Andrey Coutinho Bila kuaga

Kuna mataifa hapa ulimwenguni soka limejikita sana na kugeuka ni kama sehemu ya utamaduni wao.

Brazili na Uingereza nje ya maendeleo katika sekta nyingine lakini uwekezaji katika soka na mafanikio waliyonayo yanawapa fursa ya kutambulika kama mihimili ya soka duniani.

Brazili wakitamba kitaifa lakini Uingereza kwa misingi ya Iigi bora na maendeleo ngazi ya vilabu.

Sasa tuje kwenye mada husika baada ya kupata utangulizi huo hapo juu kutambua thamani ya soka.

Hali hii inawafanya wachezaji na wadau wa soka toka nchi hizo kuonesha umakini mkubwa katika misingi ya soka bora. Hii ikiwa na utayari wao Kisaikolojia.

Toka ametua Yanga SC Andrew coutinho alionesha uwezo asilia na si soka la kufundishwa tu. Hili liliteka nafsi za wadau wa soka .

Wapo waliohoji kwa uwezo wa Andrey amefata nini Bongo? Hii ilikuwa ni kupima uwezo wetu kisoka na uwezo wa mchezaji huyo akibebwa sana na historia ya nch yake. 

Andrey Coutinho

 Mpira ni sehemu ya utamaduni wa kinda hili na ndio maana muda mwingi alikuwa akionesha nia ya mashabiki kutaka kumpa sapoti yeye na timu yake awapo uwanjani kwa kushangilia muda wote.

Nguvu na uchanga katika ligi za ushindani zimetumika mara kibao kumuhukumu kinda huyu. 

Hakuna aliyewahi kushuku uwezo wake kwa maana ya skills. Lakini tazama mchango wa kinda huyo ndani ya klabu hiyo.

Kuna mechi lukuki Coutinho licha ya kuwekwa benchi muda mrefu lakini kila akipata wasaa aliweza kubadili matokeo ama kubadili aina ya uchezaji wa timu.

Mechi inayokumbukwa vizuri ni mechi ya juzi tu kati ya Yanga na Toto Africa. Yanga ilipotea kipindi cha kwanza lakini alipoingia kipindi cha pili game iligeuka.

Kwanini Yanga itafakari kuondoka kwake?

Coutinho aliipenda na bado anaipenda sana yanga sc. Matukio kadhaa aliofanya juu ya klabu hiyo yalitosha kuonesha mapenzi ya dhati na klabu hiyo.

Coutinho baada ya likizo ya kuchukua ubingwa wa 2014/15 akiwa likizo nchini Brazil alifanya part kubwa akiwavisha jezi ndugu na rafiki zake , jezi za Yanga. Yanga ilipata promo kitaifa.

Couinho alilia sana kuaminika na kocha ili apate nafasi ya kucheza mara kwa mara ili azoee mazingira ya ligi na kukomaa katika nguvu na soka la ushindani.

Hili liligeuka ndoto hasa msimu huu kwa kuletwa wachezaji wapya wa pembeni kama Mwashuiya, Kaseke na Malimi.
Fununu za kuuzwa St George wakati wa likizo vilianza kuua taratibu uzalendo wake kwa klabu.

Kama Yanga ingemjenga Kisaikolojia na kimbinu kwa program maalumu sidhani kinda huyu angeondoka bure kiasi hiki.

Yanga itake isitake hapa imekula hasara ya mwaka. Lini itajifunza klabu hii kusimamia misingi ya soka la kisasa?

Yanga iliwapasa toka awali kutambua utajiri wa kipaji cha Coutinho aidha kwa kuitumikia klabu kwa asilimia 100 au kwa kumtunza vyema kwa mauzo ya baadae.

Kutoka Brazil ilikuwa ni trade mark tosha kupata mlahaba kimataifa.

Ni rahisi kusema kutoroka kwa mchezaji huyu ni kavuja mkataba wake lakini mnakumbuka alivyoondoka Nonda Shaabani? na maisha baadae yakawaje?

Hapa ndipo ninaposema tuige tamaduni za wabrazil na waingereza wanavyoendesha soka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *