Yafahamu majeraha aliyoyapata Mbwana Samatta

Mbwana Samatta.

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania na mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki nne hadi sita kutokana na kupata majeraha katika goti lake la mguu wa kulia.

Samatta alipata maumivu hayo ya goti wiki iliyopita wakati akiitumikia timu yake ya  Genk dhidi ya Lokeren na kulazimika kutolewa nje ya uwanja katika dakika ya 40.

Maumivu ya Samatta ambayo kwa lugha ya kitabibu hujulikana kama, Meniscus, yaani  misuli na mifupa miepesi hutibika baada ya kufanyiwa upasuaji kama maumivu yanaonekana kuwa makubwa.

Kwa mujibu wa daktari Tumaini John kutoka Hospitali ya Alexia, jijini Dar es Salaam ameiambia Soka360 kwamba maumivu hayo mara nyingi huwapata wanamichezo wa michezo mbali mbali ukiwemo mchezo wa soka na riadha.

Picha ya goti la mwanadamu kwa ndani.

Daktari huyo amesema kwamba majeraha mengi yanayolihusu goti huweza kutibika kwa kupumzika muda mrefu, kuweka barafu kama maumivu ni mepesi lakini kwa maumivu yalikua makubwa ni lazima upasuaji ufanyike.

“Mara nyingi huwapata watu wa mikikimikiki, sana wanariadha na soka, unaweza kutibika kwa kupumzika muda mrefu, kuwekewa barafu au kufanyiwa upasuaji kwa maumivu makubwa,” alifafanua.

Majeraha ya goti yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni yale ya muda mrefu au yale ya muda mfupi, Soka360 inaungana na watanzania wote kumuombea nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta arejee uwanjani mapema.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *